Le Pen hana upande duru ya pili Ufaransa

Kiongozi wa Ufaransa wa National Front Marine Le Pen ameapa kutoandika chochote kwenye karatasi ya kupigia kura katika duru ya pili ya uchaguzi wa Urais nchini Ufaransa.

Bi Le Pen aliuambia mkutano wa hadhara mjini Paris kuwa hatamuunga mkono yeyote si Rais Nicolas Sarkozy wala mgombea wa Kishoshalist Francois Hollande na akawaambia wafuasi wake kufuata utashi wao wenyewe.

Bi Le Pen alipata kura 6.5 million sawa na 17.9% -katika duru ya kwanza ya uchaguzi.

Kura za hivi karibuni za maoni zinaonyesha kuwa Bw Hollande anaongoza kwa kura sita hadi kumi dhidi ya Bw Sarkozy.

Bw. Hollande na Bw Sarkozy watapambana uso kwa uso katika mjadala wa uchaguzi utakaotangazwa katika televisheni siku ya Jumatano.