San Suu Kyi ahudhuria kikao cha bunge

Kiongozi wa upinzani na mkereketwa wa kidemokrasia nchini Burma, Aung San Suu Kyi, ameingia bungeni kuchukua kiti chake, mwezi mmoja tu baada ya chama chake kujizolea viti vingi katika uchaguzi wa duru ya pili.

Chama cha mwanaharakati huyo kimefutilia mbali vitisho vyake vya kususia vikao vya bunge kufuatia maneno katika kiapo cha bunge waliyotaka yabadilishwe.

Chama chake cha NDL kimesema kimeamua kubadilisha msimamo wake kwa manufaa ya raia wa Burma.