Watu saba wauawa Kabul

Wanamgambo wa Taleban wamesema kuwa wameshambulia eneo moja lenya ulinzi mkali katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul.

Wengi wa waliouawa ni raia ambao walikuwa wakitoka katika shule moja karibu na eneo hilo.

Ripoti zinasema kuwa walipuaji wawili wa kujitoa mhanga walifanya mashambulio hayo yaliyodumu kwa muda wa saa nne dhidi ya jengo moja linalotumiwa na raia wa kigeni na jeshi la nchi hiyo.

Shambulio hilo limetokea muda mfupi baada ya rais Barrack Obama wa Marekani kuzuru taifa hilo na kuhutubia raia wa Marekani kupitia runinga ya taifa.

Obama aliwaeleza raia wa Marekani kuwa azma ya kuliangamiza kundi la Al-Qaeda linakaribia kufanikiwa.