Gingrich ajiondoa kuwania kiti cha urais

Mwanasiasa wa Marekani Newt Gingrich, amesitisha rasmi kampeni zake za kuwania kuwa mgombea wa kiti cha urais wa chama cha Republican, katika uchaguzi wa urais utakaoandaliwa mwezi Novemba mwaka huu.

Kufuatia uamuzi huo wa kujiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho, Gingrich, ametoa fursa ndogo kwa mpinzani wake Mitt Romney, kujiongezea matumaini ya kuwa mgombea wa chama hicho cha Republican ambaye atapambana na rais Barrack Obama katika uchaguzi wa urais.

Amemtaja rais Obama kama rais mwenye siasa kali katika historia ya marais wa Marekani.