Watu kadhaa wauawa Nigeria

Watu kadhaa wameripotiwa kuuawa kwenye shambulio lililotokea katika soko moja la mifugo mjini Potiskum Kaskazini mwa Nigeria.

Walioshuhudia shambulio hilo wameiambia BBC kuwa waliona miili ya watu ikiondolewa kutoka kwa soko hilo, baada ya watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki kushambulia soko hilo kwa vilipuzi.

Mifugo wengi wanasemekana kuteketea hadi kufa.

Idara ya polisi nchini humo imesema kuwa shambulio hilo ni la kulipiza kisasi ya mauaji ya mtu mmoja ambaye alijaribu kuiba mifugo katika soko hilo.

.