Marekani yatibua njama ya kulipua ndege

Maafisa nchini Marekani wanasema kwa ushirikiano na washirika wao kwingineko, wamefanikiwa kutibua njama ya kulipua ndege ya Marekani.

Njama hiyo inadaiwa kuhusisha kilipuzi sawa na kile kilichotumiwa na mshambuliaji aliyejaribu kulipua ndege ya shirika moja la Marekani iliyokuwa ikitoka Yemen kuelekea Marekani mwaka 2009.

Maafisa wanasema jaribio hilo lilikuwa limepangwa na kundi moja lenye uhusiani na kundi la al-Qaeda nchini Yemen, na lilipangwa kutekelezwa katika siku ya maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kuuawa kwa Osama Bin Laden.

Kilupizi hicho kinafanana na bomu ambayo ilipatikana kwenye chupi ya kijana mmoja raia wa Nigeria aliyefanya jaribo la kulipua ndege mjini Detroit wakati wa mkesha wa krismasi mwaka wa 2009.