Njama ya kulipua ndege ya Marekani

Ripoti kutoka Marekani zinasema kuwa mtu anayetuhumiwa kuhusika na njama ya kulipua ndege ya Marekani, ambayo ilitibuliwa hivi karibuni, alikuwa ni afisa wa ujasusi aliyeajiriwa na mataifa mawili.

Maafisa wa serikali ya Marekani wamenukuliwa wakisema kuwa mtu huyo alikuwa mfanyakazi wa idara ya ujasusi nchini Marekani na Saudia Arabia.

Kifaa hicho kilichonuiwa kutekeleza shambulio hilo kimesemakana kuwa sawa na kile kilichotumiwa katika jaribio la mashambulio ya Al qaeda dhidi ya ndege ya Marekani mwaka 2009.