Uchaguzi wa wabunge Algeria wasusiwa

Raia wa Algeria wameanza kushiriki katika zoezi la upigaji kura kuchaguwa wabunge wapya.

Zoezi hilo linatarajiwa kushuhudia idadi ndogo ya wapigaji kura na kuna wasiwasi kwamba uchaguzi huo hautakuwa wa huru na haki.

Lakini serikali imeahidi kuandaa uchaguzi wenye demokrasia zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini humo, huku wachunguzi wa kimataifa wakiwahimiza raia wa Algeria kupiga kura.

Makundi ya vyama vipya vya kisiasa vinashiriki katika uchaguzi huu, lakini wengi wa wagombea wao wanauhusiano wa karibu na chama tawala au na serikali.