Milipuko mikubwa Damascus,Syria

Milipuko miwili mikubwa, iliyotegwa kwenye gari, imetokea katika mji mkuu wa Syria, Damascus.

Maafisa wanasema takriban watu 40 wameuwawa na zaidi ya 100 kujeruhiwa.

Mwandishi wa BBC aliyeko katika eneo la tukio amesema kuwa milipuko hiyo ndiyo kubwa zaidi kutokea mjini Damascus, tangu maasi yaanze.

Televisheni ya kitaifa imeelezea mashambulio hayo kuwa ya kigaidi, lakini upinzani imelaumu serikali.