Dawa mpya ya ukimwi yakubaliwa

Aina moja ya dawa iliyothibitishwa kuwa na uwezo wa kuzuia maambukizi ya virusi vya HIV imepiga hatua muhimu ya kukubalika kutumika nchini Marekani.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Alama ya siku ya Ukimwi duniani

Jopo la washauri wa serikali ya marekani wameidhinisha matumizi ya dawa aina ya Trevada kwa watu walio katika hatari kubwa ya maambukizi ya virusi vya HIV-ambavyo huvuruga kinga ya mwili.

Dawa hiyo Trevada imekuwa ikitumiwa na watu waliona virusi vya ukimwi nchini Marekani tangu mwaka wa 2004.

Utafiti umeonyesha kuwa dawa hiyo inaweza kuwanga watu wasiokuwa na virusi vivyo dhidi ya maambukizi.