Gesi zaidi yagunduliwa Tanzania

Makampuni ya nchi za magharibi zimegundua kiwango kikubwa cha gesi katika ufo wa pwani ya Msumbiji na Tanzania.

Tangazo hili limetolewa na makampuni ya Italia na Uingereza ENI na BG na kusema kuwa kiwango hicho cha gesi kinatosheleza biashara ya gesi kwa soko la Asia.

Hapo nyuma ilitangazwa kugunguliwa kwa gesi na mafuta ghafi nchini Uganda, Kenya na Somalia na kuna taarifa kuwa huenda malia sioli hiyo pia ipo nchini Ethiopia.