Mapigano mapya Libya

Takriban watu saba wameuawa katika makabiliano mapya nchini Libya katika eneo la Ghadames kusini magharibi mwa nchi hiyo.

Maafisa wanasema kuwa watu waliokuwa wamejihami na wanaoaminika kutoka kabila la Tuareg ,walipambana na wenyeji wa mji huo ulio mpakani mwa Libya na Algeria.

Wanasema kuwa mambapano yalizuka kuhusu nani asimamie kizuizi cha polisi kilichoko viungani mwa Ghadames,ambacho kinafungua njia ya kuingizia bidhaa haramu.

Watawala wa muda wa Libya wanakabiliwa na wakati mgumu kudhibiti makundi ya kikabila ya nchini humo hasaa baada ya mapinduzi ya kiraia yaliyofanyika dhidi ya utawala wa aliyekuwa rais Muamar Gadafi.