WHO: Tisho kubwa la saratani na kupooza

Imebadilishwa: 16 Mei, 2012 - Saa 12:23 GMT

Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema watu wengi zaidi katika maeneo yote duniani wako katika hatari ya kupata ugonjwa wa kupooza, maradhi ya moyo na saratani.

Ikichapisha takwimu zake za mwaka kutoka nchi zote wanachama 194, WHO imesema hali kama za shinikizo la damu na unene wa kupita kiasi vinaongezeka kutokana na watu kula vyakula vingi vya mafuta, sukari na chumvi na kushindwa kufanya mazoezi.

Asilimia kumi na mbili ya watu wote duniani wanakabiliwa na unene wa kupita kiasi.

Lakini WHO imesema vifo kwa kina mama wanaojifungua na watoto vimepungua kwa kiasi kikubwa, kufuatia kampeni za chanjo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.