Guangcheng aelekea kupata paspoti

Mwanaharakati wa Uchina ambaye mwezi uliopita alikimbilia katika ubalozi wa Marekani mjini Beijing amesema Uchina imemkubalia yeye na familia yake kupatiwa hati za kusafiria katika muda wa siku kumi na tano zijazo.

Chen Guang-cheng amesema maafisa wa Uchina walimtembelea hospitalini ambako anapokea matibabu.

Mwandishi wa BBC mjini Beijing amesema hiyo ni ishara kwamba Bwana Chen ataondoka nchini humo hivi karibuni.

Maafisa wa Marekani wamekuwa wakiitaka Uchina kumruhusu mwanaharakati huyo kwenda Marekani ambako amepatiwa nafasi ya masomo katika chuo kikuu.