Kesi ya Ratkom-Ladic yaakhirishwa ghafla

Taarifa za hivi karibuini zinasema kuwa kesi ya uhalifu wa kivita dhidi ya Ratko Mladic iliyotarajiwa kusikilizwa kesho imeahirishwa ghafla .

Taarifa moja inasema jaji amechukua uamzi huo kutokana na makosa yaliyofanywa na waendesha mashtaka katika kutoa ushahidi wao.

Waendesha mashtaka leo walitarajia kumshitaki kuhusu mauaji ya Srebrenica ya mwaka 1995.

Jenerali Mladic anashutumiwa kuongoza mauaji hayo , lakini amekanusha shutuma hizo.

Katika taarifa yake ya ufunguzi wa kesi hiyo mwendesha mashtaka Peter McCloskey alielezea kile kilichogeuka kuwa maasi makubwa kuwahi kutokea barani ulaya tangu vita vikuu vya pili vya dunia.