Al Qaeeda yalaumiwa kwa mashambulizi

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon , amesema kuwa anaamini Al-Qaeda ndio walioandaa mashambulio mawili yaliyofanyika wiki iliyopita katika mji mkuu wa Syria Damascus.

Takriban watu hamsini na watano waliuawa katika milipuko mikubwa, katika shambulio baya zaidi kuwahi kupiga mji huo tangu kuanza kwa harakati za kudai mageuzi dhidi ya rais Bashar al-Assad .

Maafisa wa Syria wamekuwa wakiwashutumu mara kwa mara wapinzani kushirikiana na Al-Qaeda, huku upinzani ukiishutumu serikali kupanga mashambulio.

Jumamosi kundi lisilo maarufu la wanamgambo lenye uhusiano na Al-Qaeda lilisema lilifanya mashambulio hayo.