Mabenki ya Uhispania yashuswa hadhi

Shirika la kupima viwango la Moody limezishushia hadhi benki kumi na sita huku kukiwa na hofu juu ya mdoror wa kiuchumi katika muungano wa nchi zinazotumia sarafu ya Euro.

Likiangazia mdororo wa uchumi unaoendelea nchini Uhispania, Shirika la Moody's limetaja kupungua kwa uwezo wa serikali wa kushughulikia wadeni wake .

Awali viwango vya hisa katika benki ya tatu kwa ukubwa nchini humo Bankia, ziliporomoka baada ya taarifa kuwa wateja wamekuwa wakiharakisha kutoa akiba zao.

Waandishi wa habari wanasema kuna hofu kuwa benki za Hispania ziko katika hatari ya kufilisika kiasi kwamba serikali ya nchi hiyo itashindwa kuzipatia dhamana.