Picha inayomkajeli rais Zuma

Chama tawala nchini Afrika Kusini ANC, kimesema kinachukua hatua za kisheria kulazimisha nyumba moja ya sanaa ambayo inaonyesha picha ya rais Jaocob Zuma, sehemu zake za siri zikiwa nje kuondoa mchoro huo.

Msemaji wa chama ametaja picha hiyo kama inayoudhi, ya kuchukiza na yenye matusi.

Mchoro huo ni sehemu ya maonyesho ya michoro mjini Johannesburg yenye kauli mbiu ' Sifa kwa mwizi' na ambayo inajumuisha michoro yenye lengo la kukosoa chama tawala ANC.

Mchoraji wa picha hiyo Brett Murray, alisema kuwa picha zake zenyewe zinajieleza.