Ukiukwaji wa haki za wahamiaji Angola

Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Human Rights Watch, limetuhumu vikosi vya usalama vya Angola kwa kubaka na kutesa wanawake na wasichana nchini humo.

Shirika hilo linasema kuwa visa hivyo vilitokea wakati wa shughuli ya kuwarudisha makwao wahamiaji haramu kutoka Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Kwa mujibu wa shirika hilo watafiti wake walisikia ushahidi wa ubakaji kutoka kwa mwathirika baada ya mwingine kuhusu walivyobakwa, kuteswa na kudhulumiwa.

Zaidi ya watu miambili walielezea walivyoteswa.

Hata hivyo serikali ya Angola haijajibu tuhuma hizo.