Makabiliano mapya mjini Beirut

Mapigano mapya yametokea katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut, kwa mara ya kwanza ambapo wafuasi na wapinzani wa Rais wa Syria, Bashar al-Assad wamepigana kwa masaa kadhaa.

Watu kadhaa wanadaiwa kuuawa katika maeneo yanayokaliwa na Wasunni wengi.

Vizuizi vya tairi vinavyoteketea vilifunga barabara kadhaa kabla maafisa wa usalama wa Leanon kuingilia na kudumisha amani.

Mapigano hayo yalizuka kufuatia kupigwa risasi kwa wahubiri wawili maarufu wa Kisuni wanaowaunga mkono wapiganaji wanaompinga Rais Al-Assad.

Viongozi hao wa kidini waliuliwa Jumapili.

Mwandishi wa BBC mjini Beirut amesema matukio hayo yanaonyesha jinsi watu walivyogawanyika kuhusiana na mzozo wa syria.