Al Meghrai kuzikikwa Libya

Mtu wa pekee aliyehukumiwa kwa shamulizo la bomu dhidi ya ndege Marekani katika anga ya Lockerbie mwaka 1988 anatajiwa kuzikwa hivi punde nchini Libya.

Abdelbaset al-Megrahi alifariki mjini Tripoli siku ya Jumapili. Megrahi alikuwa anaugua saratani na alikuwa ameachiliwa huru kutoka jela nchini Scotland miaka mitatu iliyopita.

Alikanusha kuhusika na shambulio hilo dhidi ya ndege hiyo, shambulizi ambalo lililosababisha vifo miambili na sabini.

Marekani imesema itashirikiana na washirika wake wapya nchini Libya kuwakamata wote waliohusika.

Maafisa wa utawala nchini Libyawamwambia vyomvo vya habari kuwa wako tayari kushirikiana na Marekani wakisema wanataka kuvumbua kila walichokiita uhalifu wa aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Muammar Gaddafi