Mbakaji wa watoto ahukumiwa

Mtu mmoja aliyewabaka watoto nchini Uholanzi , amehukumiwa kifungo cha miaka kumi na mimane gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kuwabaka watoto sabini waliokuwa chini ya ulinzi wake.

Robet Mikelsons, mzaliwa wa Latvia, alifanya uhalifu huo wakati alipokuwa ameajiriwa katika vituoviwili vya malezi ya watoto mjini Amsterdam.

Baadhi ya waathiriwa wakuwa watoto wa miezi kadhaa.

Mtu huyo mwemye umri wa miaka 28, alimwagia maji jaji aliyetoa hukumu hiyo na hata kumtusi wakati akipewa hukumu yake.

Robert pia atapokea matibabu ya kiakili.