Polisi wafungwa jela Misri

Mahakama nchini misri imewafunga gereza polisi watano kwa muawaji ya waandamanji wakati wa mapinduzi ya kiraia dhidi ya aliyekuwa rais Hosni Mubarak mwaka 2011.

Watano hao wamehukumiwa kifungo cha miaka kumi gerezani.

Maafisa wengine wawili wamepewa kifungo cha mwaka mmoja kilicho-akhirishwa lakini wengine kumi wakaondolewa mashtaka.

Hiyo ni hukumu ya kwanza kwa maafisa wa polisi ambao walilaumiwa pakubwa kwa mauaji ya mamia ya waandamanaji wakati wa maandamano ya mwaka jana.

Waandamanaji watano waliuwawa huku wengine kumi na saba wakijeruhiwa mnamo tarehe 28 na 29 Januari mwaka mwaka jana.