Nchi sita kukutana kuhusu nyuklia Iran

Wajumbe kutoka mataifa sita yenye ushawishi mkubwa duniani wanatarajiwa kukutana kwa awamu mpya ya mazungumzo na Iran kuhusu mpango wake wa nuklia.

Mazungumzo hayo yanafanyika katika mji mkuu wa Iraq Baghdad, kufuatia ombi la serikali ya Iran.

Wanachama watano wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa na Ujerumani watajaribu kushawishi wajumbe wa Iran kuelezea kuhusu mipango ya nuklia ya serikali yake.

Mataifa ya magharibi yamedai kuwa Iran ina njama ya kuunda zana za kitonoradi, madai ambayo yamepingwa vikali na Tehran.

Iran imesema mpango wake wa nuklia ni wa kuzalisha nishati.