Maelfu waendelea kukimbia vita Sudan

Mapigano nchini Sudan kati ya wanajeshi wa serikali na waasi kusini mwa nchi hiyo yanawalazimisha maelfu ya watu kuvuka mpaka na kuingia Sudan kusini.

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa,limesema kuwa idadi ya watu waliotoroka jimbo la Blue Nile, imeongezeka kutoka watu elfu moja miatano hadi elfu kumi katika wiki chache zilizopita.

Kwa mujibu wa shirika hilo, hali ya watu hao ni mbaya sana.

Indaiawa kuwa waasi wa kundi la SPLM-North hivi karibuni waliunda ushirikiano na makundi mengine ya waasi kwa lengo la kupindua serikali ya Khartoum.