Musri aahidi kujumuisha wote, Misri

Mgombea wa urais kwa chama cha Muslim Brotherhood nchini Misri Mohamed Mursi, amesema atajumuisha makundi yote ya kisiasa kwenye serikali yake endapo atashinda duru ya pili ya uchaguzi wa urais.

Katika taarifa iliyoangazia makundi yanayohofia utawala wa mrengo unaoegemea sera za kiisilamu.

Bw. Musri amesema atajumuisha wanawake na vijana akisema kila anataka ni kumaliza uatwala wa kiimla na kuweka taasisi thabiti za utawala.

Awali makao makuu ya mshindani mkuu wa Musri, Ahmed Shafia ambaye alihudumu kama Waziri Mkuu kwenye uliokuwa utawala wa Rais Mubarak yalishambuliwa.