Jullian Assange kuhamishiwa Sweden

Mahakama ya Juu Uingereza imeidhinisha kuhamishwa kwa mwanzilishi wa wavuti wa Wikileaks Julian Assange kutoka Uingereza hadi Sweden ambapo anakabiliwa na kesi ya udhalilishaji wa ngono.

Majaji wengi kati ya watano waliosikiliza rufaa ya bw. Assange walipinga.

Mawakili wa Assange wanasema kibali cha Sweden siyo halali.

Wafuasi wa Bw Assange wanahofia Sweden huenda ikamkabidhi kwa Marekani ambapo anatakikana kwa mashtaka kuhusiana na kuchapisha nyaraka hizo za siri.

Assange ana majuma mawili kukata rufaa.