Wanaharakti waishtaki serikali Uganda

Mahamaka moja nchini Uganda imetupilia mbali kesi iliyowasilishwa na kundi la wanaharakati wa kike dhidi ya Serikali kwa kile waliochokiita vifo vya akina mama waja wazito ambavyo vinaweza kuepukika.

Mahakama hio ya kikatiba iliamua kuwa hilo lililikuwa na swala la kisiasa na wala sio kisheria.

Wanaharakati wameituhumu serikali kwa kukiuka haki za kikatiba kwa kukosa kuwapa wanawake wajawazito vifa na huduma bora wakati wa kuzaa. KUNDI -- lililoasilisha kesi hio mwaka uliopita -- limesema litakata rufaa.