Mwanamgambo wa Al Qaeeda alengwa

Afisa mmoja mwandamizi wa serikali ya marekani ameiambai BBC kuwa mwanamgambo mmoja Abu Yahya al-Libi, ambaye anakisiwa na utawala wa washington kuwa naibu kiongozi wa kundi la al Qaeda, alilengwa kwenye shambulio la anga lililofanywa na wanajeshi wake nchini Pakistan hiyo jana.

Afisa huyo hata hivyo hajasema ikiwa mwanamgambo huyo Abu Yahya al-Libi ambaye ni msomi kutoka Libya aliuawa wakati wa shambulio hilo.

Ripoti kadhaa zimesema kuwa Al Libi, alikuwa emeuawa kwenye shambulio lingine lililofanywa decemva mwaka wa 2009, lakini habari hizo zilibainika kuwa hazikuwa za kweli.