Mchezaji Mpalestina hali mbaya Israel

Makundi ya kutetea haki za binadamu yameonya kuwa mchezaji soka wa Palestina ambaye amesusia kula kwa siku themanini sasa akiwa katika jela ya Israel huenda akafariki dunia.

Mahmoud Sarsak ambaye wakati mmoja alikuwa mchezaji nyota wa timu ya taifa ya Palestina amekuwa jela kwa muda wa miaka mitatu bila kufikishwa mahakamani au kushtakiwa.

Shirika la Amnesty International limetoa ripoti kushtumu tukio hilo. Bwana Sarsak ni mmoja wa wafungwa wa Palestina ambao wamekataa mpango uliofikisha kikomo kususia chakula mwezi uliopita.