Uchunguzi wa viungo unaendelea Canada

Luka Rocco Magnotta Haki miliki ya picha AFP
Image caption Luka Rocco Magnotta

Polisi nchini Canada wamesema kuwa viungo vya mwili vilivyotumwa kwa shule mbili mjini Vancouva, huenda vilitoka kwa mwili sawa na viungo vingine viwili vilivyotumwa kwa vyama vya kisiasa, lakini uchunguzi wa DNA unahitajika ili kuthibitisha madai hayo.

Viungo hivyo vinashukiwa kutoka kwa mwili wa Jun Li, mwanafunzi mwenye asili ya kichina aliyeuawa na mpenzi wake, Luka Rocco Magnotta ambaye anashukiwa kumuua na kutakata mwili wake mjini Montreal, ambako polisi wanasema viungo hivyo vilitumwa

Mchezaji huyo wa filamu za ngono alikamatwa na polisi mapema wiki hii nchini Ujerumani na anatarajiwa kusafirishwa hadi Canada ili kufunguliwa mashtaka.

Magnota anaripotiwa kumuua Lin na kuchapisha picha zake katika mtandao wa internet.