Panetta awasili Afghanistan

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Haki miliki ya picha AP
Image caption Waziri wa Ulinzi wa Marekani

Waziri wa ulinzi wa Marekani, Leon Panetta, amewasili nchini Afghanistan katika ziara ambayo haikuwa imetangazwa.

Panetta amewaambia waandishi wa habari kuwa, anataka kusikia tathmini ya hali ilivyo nchini humo kutoka kwa makamanda hususan kuhusu kuongezeka kwa visa vya mashambulio na mipango ya kuondoa wanajeshi nchini Afghanistan.

Panetta, amesema mashambulio hayo ya wanamgambo ya hivi karibuni yameonekana kupangwa, lakini amekariri kuwa viwango vya ghasia nchini Afghanistan vimepungua vikilinganishwa na miaka iliyopita.

Hapo jana zaidi ya raia 20 waliuawa kwenye shambulio lililotekelezwa na mlipuaji wa kujitoa mhanga nje ya kambi moja inayotumiwa na wanajeshi wa muungano NATO Kusini mwa nchi hiyo.