Dudus Coke jela miaka 23

Mahakama mjini New York Marekani imemhukumu mlaguzi wa dawa za kulevya kutoka Jamaica Christopher Dudus Coke miaka 23 gerezani.

Coke alikiri makosa ya ulaghai na kuchochea vurugu.Alihamishwa kutoka Jamaica miaka miwili iliyopita baada ya makabiliano makali kati ya genge tiifu kwake na wanajeshi katika kitongoji kimoja mjini Kingstone Jamaica.

Karibu watu 70 walikufa katika makabiliano hayo.