Ndoa ya lazima yapigwa marufuku UK

Kumlazimisha mtu kuoa au kuolewa kinyume na hiari yake huenda sasa ikiwa kitendo cha uhalifu nchini Uingereza, Wales na Ireland ya Kaskazini.

Haya ni kwa mujibu wa mapendekezo mapya yatakayotangazwa na serikali ya Uingereza baadaye hii leo.

Inakadiriwa kuwa kuna kati ya waathiriwa elfu tano na nane waliolazimishwa kuoa au kuolewa nchini Uingereza.

Wasichana wengi wanaolazimisha kuolewa wana umri wa chini ya miaka 21 lakini kuna ripoti kuwa wasichana wa hata umri wa miaka15 hulazimishwa kuolewa.

Familia nyingi zinazotuhumiwa kutekelEza uhalifu huo zinatoka mataifa ya bara Asia hususan taila la Pakistan.