Polisi Japan waimarisha msako

Maelfu ya polisi nchini Japan wanaendela na shughuli ya kumtafuta mshukiwa mmoja, ambaye anatuhumiwa kuwa miongoni mwa waaumini wa dhehebu moja haramu waliotekeleza mauaji ya kishirikina, kwa kutumia gesi ya sumu, katika barabara ya chini ya ardhi nchini humo.

Maafisa hao wamekuwa wakisambaza picha za mshukiwa huyo, kwa Jina Katsuya Takahashi, amabye anaripotiwa kutoweka kutoka kwa nyumba yake muda mfupi kabla ya kuvamiwa na polisi siku ya jumatatu.

Mshukiwa huyo amekuwa mafichoni tangu shambulio hilo lililotekelezwa na watu wa dhehebu la Aum Shinrikyo mwaka wa 1995.

Mshukiwa mwingine Naoko Kikuchi mwenye umri wa miaka 40 alikamatwa mjini Kawasaki siku ya Jumapili.