Waangalizi wafika Qubair Syria

Waangalizi wa Umoja wa Mataifa wameingia katika kijiji cha Qubair, ambako kulifanyika mauaji ya raia Jumatano wiki hii.Mwandishi wa BBC aliyeandamana na waangalizi hao ameelezea eneo hilo kama la kusikitisha sana.

Nyumba moja anasema mwandishi huyo ilikuwa na ubongo wa watu na damu, huku makaazi mengine yakiwa na haurufu ya nyama za binadamu walioteketezwa.

Hawakupata maiti zozote.Kundi dogo la waangalizi limesalia katika kijiji hicho ambapo wamegundua magari ya kijeshi yamekuwa yakizuru eneo hilo.