Kisiwa cha Falklands kuamua mustakhabali

Raia wa kisiwa cha Falklands ambacho ni himaya ya Uingereza na kudaiwa na Argentina kama eneo lake watafanya kura ya maoni mwaka ujao kuamua mustakabhali wao wa kisiasa.

Kiongozi wa serikali ya Falklands amesema Kura ya maoni itatoa ujumbe kwamba wanakisiwa hao wanataka kusalia kuwa himaya ya Uingereza.

Ameongeza Argentina haina haki kupinga matakwa ya raia wa kisiwa hicho.

Uingereza na Argentina zilipigana vita dhidi ya udhibiti wa kisiwa hicho miongo mitatu iliyopita baada ya majeshi ya Argentina kuvamia Falklands lakini baadaye yakalazimika kuondoka.

Serikali ya Uingereza imeunga mkono kufanyika kura hiyo ya maoni.