Ni vita vya wenyewe kwa wenyewe Syria

Mkuu wa waangalizi wa Umoja wa Mataifa nchini Syria Herve Ladsous amesema machafuko nchini humo ni yamefikia kiwango cha kutajwa kama vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Hii ni mara ya kwanza afisa wa uangalizi wa Umoja wa Mataifa ameelezea rasmi hali halisi nchini humo.

Bw Ladsous amesema serikali ya Syria imepoteza maeneo mengi kwa makundi ya waasi huku vita zikiendelea kuchacha.

Shirika la msalaba mwekundu linasema haliwezi kukidhi mahitaji ya kibinadamu. Shirika hilo ndilo pekee linalohudumu ndani ya Syria.