Syria yatuhumiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu

Katika ripoti mpya ya shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International, serikali ya Syria imeshutumiwa kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.

Amnesty International wanasema, watafiti wake wamezungumza na wakaazi zaidi ya mia mbili katika miji ishirini na tatu na vijiji nchini Syria tangu katikati ya mwezi Aprili; na limeishutumu serikali ya Syria kwa kuendesha sera ya kuunguza mazao na nyumba katika baadhi ya maeneo yenye uvamizi, kwa kuwaua au kuwatesa raia, na kuua mifugo.

Katika mji wa Aleppo, watafiti wa Amnesty waliona vikosi vya serikali ya Syria na wanamgambo washirika wake kwa kuyafyatulia risasi maandamano ya amani, na kuwaua na kuwajeruhi waandamanaji na wapita njia.

Afisa mwandamizi mshauri wa migogoro katika shirika la Amnesty, Donatella Rovera, amesema serikali ya Syria imekuwa ikiwalenga hususan raia na kwa makusudi: