Mkutano kuhusu mpango wa nuklia wa Iran

Viongozi wa dunia wanakutana tena kwa mazungumzo na Iran kuhusu mpango wake wa nuklia huku kukiwa na wasiwasi kuwa nchi hiyo inanuia kuunda zana za nunklia.

Iran inatakiwa kupunguza mradi wake wa kurutubisha madini ya uranium hadi asilimia ishirini na hata kufunga mojawapo ya viwanda vyake vya Uranium vilivyoko chini ya ardhi.

Kwa upande wake, Iran inataka vikwazo dhidi yake kusitishwa na kutaka kukubalika kwa kile inachotaja kama haki yake ya kurutubisha madini ya Uranium kwa matumizi salama.

Msemaji wa mwakilishi wa muungano wa Ulaya kwenye mazungumzo hayo, alisema kuwa hali wakati wa kuanza kwa mazungumzo mjini Moscow ilikuwa nzuri tu.