Rais Francois Hollande ana wabunge wengi

Chama cha Kisosholisti cha rais mpya wa Ufaransa, Francois Hollande, kimenyakuwa wingi wa viti katika bunge kwenye duru ya pili ya uchaguzi.

Duru hiyo ya pili na ya mwisho ya uchaguzi iliyofanyika jana Jumapili ilikipa chama hicho zaidi ya viti mia mbili themanini vinavyohitajika kuthibiti bunge.

Waziri mkuu kutoka chama cha Kisosholisti, Jean-Marc Ayrault, alisema azma iliyopo kwa sasa ni kuelekeza ulaya katika mkondo wa ukuaji ili kulinda Ukanda wa Euro.

Chama cha mrengo wa kulia National Front kilinyakuwa viti vya ubunge kwa mara ya kwanza baada ya kipindi cha miaka kumi na tano--lakini mshirika wa zamani wa bwana Hollande, Segolene Royal, alishindwa katika uchaguzi huo.