Polisi 3 wauawa nchini Afghanistan

Maafisa watatu wa polisi wameuawa kusini mwa Afghanistan kufuatia shambulio lililotekelezwa na wanamgambo.

Wanamgambo waliokuwa wamevalia sare za polisi walishambulia kituo kimoja cha ukaguzi na kuwaua maafisa watatu wa polisi.

Maafisa wa serikali ya nchi hiyo pia wamesema raia wanane waliuawa, sita kati yao wakiwa watoto kwenye shambulio hilo lililotokea katika mkoa wa Helmand.

Ripoti zinasema raia hao walikuwa wakisafiri kwa gari wakati bomu lililokuwa limetegwa kandO ya barabra lilipolipuka.