Makabiliano kati ya jeshi na waasi Uturuki

Takriban wanajeshi wanane wa Uturuki wameuawa na wengine kumi na sita kujeruhiwa kufuatia makabiliano makali na wapiganaji wa kikurdi usiku wa kuamkia leo.

Serikali ya Uturuki imesema kundi kubwa la waasi wa PKK walivamia kituo kimoja cha kijeshi katika maeneo ya milimani kusini mashariki na nchi hiyo, karibu na mpaka wa Iraq.

Ripoti zinasema wapiganaji kumi wa waasi waliuawa kwenye shambulio hilo.