Mlipuaji wa Bali afungwa miaka 20

Mahakama moja nchini Indonesia, imemhukumu miaka 20 gerezani mshukiwa mmoja wa mashambulio ya mabomu ya Bali ambayo yalifanyika mwaka wa 2002.

Jopo la majaji lilimpata Umar Patek na hatia ya mauaji na pia ya kutengeneza mabomu yaliyotumika kulipua klabu kimoja huko Bali.

Shambulizi hilo lilisababisha mauaji ya watu zaidi ya 200.

Mtu huyo pia alipatika na hatia ya kuhusika na mauaji katika mashambulizi yaliofanywa katika kanisa moja huko Jarkata. Shambulizi hilo lisababisha mauaji ya watu 19.

Upande wa mashtaka haukuomba mahakama hiyo kutoa adhabu ya kifo baada ya Umar Patek kuomba radhi kwa kitendo chake.