Beckham hatashiriki Olimpiki

Aliyekuwa nahodha wa Uingereza, David Beckham, amekosa nafasi katika timu itakayowakilisha Uingereza wakati wa michezo ya olimpiki.

Beckham amesema hakuchaguliwa kuwa mmoja wa wachezaji katika timu hiyo inayojumuisha wachezaji kumi na wanane.

Amesema kuwa angependa kuiwakilisha Uingereza na amevunjika moyo kutoka na uamuzi huo.