Assange azidi kutafuta hifadhi Ecuador

Mwasisi wa mtandao wa Wikileaks , Julian Assange, amesisitiza kupitia msemaji wake kuwa ataendelea na juhudi zake kutaka hifadhi ya kisiasa nchini Ecuador. Wiki jana aliingai katika ubalozi wa Ecuador mjini London.

Asange anatakikana nchini Sweden kwa madai ya dhuluma ya kikongo, madai anayosema kuwa yameshinikizwa kisiasa.

Hii leo polisi wa Uingereza wamemtaka afikie katika kituo kimoja cha polisi lakini msemaji wake amesema kuwa Asange anahofia huenda akarejeshwa kwa lazima nchini Marekani na kushtakiwa kwa madai ya upelelezi.