Wanachama wa Basque wakamatwa

Polisi nchini uingereza wamewakamata wanachama wawili wa kundi la wanamgambo linalotaka kujitenga la Basque,ETA.

Serikali ya Uhispania imewataja wawili hao, Anton Troitino na Ignacio Lerin kama wanachama waandamizu wa kundi hilo.

Wawili hao walitiwa nguvuni na maafisa waliokuwa wamejihami mjini London kuhuisiana na madao ya kujihusiha na vitendo vya kgaidi vilivyotekelezwa nchini Uhispania.

Bwana Tro Teen Ehhnoh anasakwa kuhusiana na mauaji ya zaidi ya watu ishirini.

Mwaka uliopita kundi hilo la ETA lilisema kuwa litasitisha mashambulio yake lakini serikali ya Uhispania na vita vya silaha, lakini serikali ya Uhispania inasisitiza kuwa lazima kundi hilo liweke silaha zao chini.