Wabunge wapya wachaguliwa Senegal

Bunge jipya limechaguliwa nchini Senegal, miezi minne tangu rais Macky Sall kuchaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo na kumaliza utawala wa rais Abdoulaye Wade uliodumu kwa miaka kumi na miwili.

Idadi ndogo ya wapiga kura walijitokeza kupiga kura wakati wa uchaguzi huo wa ubunge.

Ufisadi ulikuwa mojawapo wa masuala yaliyoangaizwa pakubwa wakati wa kampeini.

Mwandishi wa BBC magharibi mwa afrika anasema uchaguzi huo ni zoezi la kwanza la kupima umaarufu wa rais macky sall, ambaye utawala wake umehaidi kuwaa na kurejesha mali ya fedha zote za serikalai zilizoibiwa.

Tume ya uchaguzi nchini humo imesema kuwa imeridhishwa na jinsi uchaguzi huo ulivyoendeshwa matoke rasmi yanatarajiwa kutangazwa hii leo.