Syria yajutia kudungua ndege ya Uturuki

Rais wa Syria Bashar Al Assad ameliambia gazeti moja nchini Uturuki kuwa anajuta sana, kuwa wanajeshi wake waliangusha ndege inayomilikiwa na serikali ya Uturuki mwezi uliopita.

Rais Assad amesema wanajeshi wake hawakugunduwa kuwa ndege hiyo ni ya Uturuki hadi uchunguzi ulipofanyika.

Amesema ndege hiyo ilikuwa ikipaa katika anga ambayo inalotumiwa na ndege za kivita za Israeli.