Maafisa wa Fukushima hawakuwajibika

Jopo maalum lililoteuliwa na bunge la Japan kuchunguza jinsi serikali ya nchi hiyo ilivyoshughulikia janga la Fukushima mwaka uliopita, limetoa matokeo ya uchunguzi wake hii leo.

Ripoti hiyo inasema licha ya janga hilo kusababishwa na tukio ambalo halingeepukika , ajali iliyotokea katika kiwanda cha nuklia cha Fukushima, ilisababishwa na ukosefu wa uwajibikaji.

Mwenyekiti wa jopo hilo Kiyoshi Kurokawa amesema makosa kadhaa na ukosefu wa uwajibikaji yalikifanya kiwanda hicho kutojiandaa kwa tetemeko la ardhi na Tsunami iliyotokea mwezi Machi mwaka uliopita.

Mwenyekiti wa jopo hilo, Kiyoshi Kurokawa, amesema tume yake imefanya uchunguzi wa kutosha.